Australia kukabiliwa na Joto Kali

0
515

Wakazi nchini Australia kuanzia wiki ijayo, huenda wakashuhudia joto kali wakati wa mchana, joto ambalo linatarajiwa kuweka rekodi.

Katika taarifa yake, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Australia imeeleza kuwa, joto hilo linatarajiwa kuongezeka na kufikia nyuzi joto 40 Sentigredi katika maeneo mengi ya nchi hiyo kuanzia siku ya Jumatano.

Rekodi ambayo ipo kwa sasa ni ile ya mwezi Januari mwaka 1960, ambapo mji wa Oodnadatta nchini humo ulikua na nyuzi joto 50.7 Sentigredi.

Kufuatia tishio hilo la joto kali katika maeneo mbalimbali nchini Australia, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kutokea kwa moto hasa kwenye maeneo ya Magharibi.

Wataalam wa Hali ya Hewa nchini Australia wamesema kuwa, joto hilo kali litaendelea kuongezeka na hata kufikia nyuzi joto 42 Sentigredi katika baadhi ya maeneo.