Aung San Suu Kyi kifungoni miaka minne

0
191

Mahakama ya Kijeshi nchini Myanmar imemhukumu Aung San Suu Kyi kifungo cha miaka minne jela, kutokana na makosa ya uchochezi na kuvunja sheria ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

San Suu Kyi ambaye ni kiongozi wa kiraia pamoja na Rais wa nchi hiyo Win Myint walikamatwa mwezi Februari mwaka huu baada ya jeshi kuipindua Serikali ya kiraia na kuwakamata viongozi wake na wanaharakati mbalimbali.

Maandamano yanaendelea nchini Myanmar ambapo watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa huku Jumuiya ya Kimataifa ikiendelea kuushinikiza uongozi wa kijeshi nchini humo kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa pamoja na kuresha utawala wa kidemokrasia.