Kiongozi wa Myanmar, Aun San Su Chi, tayari amewasili katika Mahakama ya Kimataifa The Hague nchini Uholanzi ili kutoa utetezi wake kuhusiana na mauaji ya watu wa kabila la Rohingya.
Nchi hiyo inatuhumiwa kufanya mauaji ya kikabila dhidi ya watu hao, waliolazimika kukimbilia nchini Bangladesh kama wakimbizi.
Maelfu ya waandamanaji wameonekana wakiandamana kupinga kiongozi huyo kufikishwa mahakama hiyo ya kimataifa baada ya Gambia kuifungulia mashtaka serikali ya myanmar katika mahakama ya makosa ya jinai The Hague dhidi ya mauaji ya kimbari ya jamii ya rohingya yaliyofanyika mwaka 1948.
