Augustino Mrema afariki dunia

0
170

Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Mrema amefariki dunia asubuhi hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mkoani Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mrema aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Pia aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR – Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi anafariki dunia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Alizaliwa Desemba 31 mwaka 1944, huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Mrema alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia tarehe 16 mwezi huu.