Arobaini na tano wafariki Dunia wakati wa Mazishi ya Jenerali Qassim

0
308

Zaidi ya watu arobaini na tano wamefariki Dunia na wengine zaidi ya mia mbili wamejeruhiwa baada ya kukanyagana katika msongamano wakati wa mazishi ya aliyekuwa kamanda wa kijeshi nchini Iran Qassim Suleiman aliyeuwawa na majeshi ya marekani wiki iliyopita nchini Iraq.

Mapema hii leo mamilioni ya waombolezaji wakiongozwa na Rais wa Iran Hassan Rouhani wamejitokeza katika mazishi ya kiongozi huyo aliyekuwa anatajwa kuwa na ushawishi ambapo
Rais Rouhan ametoa pole kwa ndugu na familia ya walioukufa pamoja na majeruhi.

Wakati huo huo kiongozi wa wanamgambo wa Iraq, Abu Mahdi al Mouhandis naye amezikwa hii leo nchini mwake.

Mwili wa Suleiman umehifadhiwa katika mji wa Kerman uliopo kusini mashariki mwa Iran alipokuwa akiishi.

Iran imeapa kulipiza kisasi mauaji hayo ya kiongozi wa jeshi Soleimani hali inayohofiwa kutokea kwa vita baina ya pande hizo mbili.