Apple Yapoteza Trilioni 21 ndani ya Saa Moja

0
489

Kampuni ya Apple imepoteza Tsh 21 Trilioni ($9bn) katika soko la hisa, saa moja baada ya Jony Ive aliyehusika katika ubunifu wa takribani bidhaa zote za Apple, kutangaza kuondoka ndani ya kampuni hiyo.

Sir Jonathan Paul “Jony” Ive, ana miaka 27 ni Mwingereza, alijiunga na Apple mwaka 1992. Baada ya miaka kumi ya huduma ya kuunda bidhaa za Apple Ive alipandishwa cheo kuwa Makamu wa Rais Mkuu wa kubuni bidhaa za Apple Ive ameunda iPod, iPhone, iPad, MacBook, na sehemu za interface ya mtumiaji wa Apple, iOS.

Ive ametangaza kufungua kampuni yake ya ubunifu, ambayo Apple itakuwa mteja wake.