Ang’atwa na nyoka aliowafuga

0
173

Zaidi ya nyoka mia moja wamegundulika katika shamba moja lililopo kwenye mji wa Salzgitter nchini Ujerumani.
 
Polisi nchini Ujerumani wamesema nyoka hao wamegundulika baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 35 anayedaiwa kuwa ni mmiliki wa shamba hilo kung’atwa na nyoka hao.

Baada ya mwanamke huyo kung’atwa na nyoka mwenye sumu kali alikwenda katika hospitali moja iliyopo karibu na mji wa Hannover na kuwaeleza madaktari kuwa mmoja wa nyoka wake amemuuma kidole.
 
Hali ya mwanamke huyo ilivyozidi kuwa mbaya, polisi walikwenda shambani kwake na ndipo walipobaini uwepo wa nyoka wengi ambao ni pamoja na chatu.
 
Nyoka hao hawakuwa wamehifadhiwa katika masanduku sahihi na hivyo kuwalazimu polisi kuwachukua wote na kuondoka nao.