Mkazi mmoja wa mji wa Columbus uliopo katika jimbo la Ohio nchini Marekani amemuua kimakosa mtoto wake wa kike Janae Hairston mwenye umri wa miaka 16, kwa kumdhania ni mhalifu aliyekuwa anavamia nyumbani kwake.
Mama wa Janae ndiye aliyepiga simu kuomba msaada baada ya tukio hilo majira ya alfajiri, akisema binti yake alikuwa amelala sakafuni kwenye gereji ya nyumba yao baada ya kupigwa risasi kimakosa na baba yake.
Wazazi wote wa binti huyo walisikika wakipiga kelele kwa sauti wakitaka mtoto wao ainuke baada ya tukio la kupigwa risasi,
Wauguzi wa dharura walifika katika nyumba hiyo kumchukua Janae na kumpeleka kwenye hospitali ya Mount Carmel East, ambapo hata hivyo alifariki dunia saa moja baadaye.