Aliyekuwa Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani amewaomba radhi raia wa nchi hiyo baada ya kukimbia nchini humo na kwenda kutafuta hifadhi Umoja wa Falme za Kiarabu.
Amesema kuondoka Afghanistan ulikuwa ni uamuzi ngumu zaidi katika maisha yake na hakuwa na nia ya kuwaacha watu wake, lakini alifanya hivyo ili kunusuru vurugu.
Ashraf Ghani aliukimbia mji wa Kabul wakati wapiganaji wa kundi la Taliban walipokuwa wakikaribia kuingia katka mji huo.
Ameongeza kuwa tuhuma za kwamba amekimbia na dola milioni 169 za kimarekani kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu si za kweli.
Ghani alilazimishwa kuondoka Afghanistan na walizi wake, kwa kuwa kulikuwa na dalili kwamba anaweza kukamatwa na kuuawa.
Mapema wiki hii wapiganaji wa Taliban ambao kwa sasa ndio wanaiongoza Serikali ya Afghanistan baada ya mapambano na vikosi vya Serikali, walitangaza baraza jipya la mpito la Mawaziri.