Al- Bashir ang’olewa

0
595

Rais  Omar Al-Bashir  wa Sudan ameondolewa madarakani na amekamatwa, baada ya kuongoza Taifa hilo kwa muda wa miaka Thelathini.

Akilihutubia Taifa kupitia kituo cha Televisheni cha nchi hiyo, Waziri wa Ulinzi wa Sudan, -Awad Ibn Ouf  amesema kuwa kwa sasa uongozi wa mpito wa nchi hiyo utakua chini ya Jeshi kwa kipindi cha miaka miwili, wakati uchaguzi wa Rais ukisubiriwa kufanyika.

Ouf ameongeza kuwa Al-Bashir yuko salama na baada ya kukamatwa amewekwa sehemu ambayo hawezi kudhurika.

Kufuatia hatua hiyo ya kuondolewa madarakani kwa Rais  Omar Al-Bashir, -Sudan imewekwa chini ya hali ya tahadhari kwa muda wa miezi mitatu.

Al Bashir ameondolewa katika wadhifa huo wa Urais kufuatia maandamano ya siku kadhaa yaliyofanywa na Raia wa Sudan waliokua wakishinikiza aondoke madarakani.