Mwanaume mmoja wa Los Angeles nchini Marekani, ambaye alikaa jela kwa takribani miaka 38 kwa kosa la mauaji ambayo hakuyafanya, ameachiliwa huru baada ya vipimo vya DNA kutoa majibu yanayomhusu mtu mwingine ambaye alikwishafariki dunia.
Maurice Hastings ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 69, alihukumiwa kwa kosa la mauaji ya Roberta Wydermyer aliyefariki dunia mwaka 1983 kwa kupigwa risasi kichwani.
Baada ya uchunguzi, mwaka 1988 Hastings alihukumiwa kifungo cha maisha jela, huku makosa yake yakitwajwa kuwa ni mauaji, unyang’anyi na unyanyasaji wa kijinsia.
Mwaka 2000 Hastings aliomba vifanyike vipimo vya DNA lakini ombi lake lilikataliwa, lakini hata hivyo hakukata tamaa aliendelea kupambania haki yake.
Wakati hukumu yake ikibatilishwa,
Hastings alionekana mwenye hisia kali na kueleza kuwa, alikuwa akisali kwa miaka mingi ili ukweli ujulikane na kuongeza kuwa anachohitaji hivi sasa ni kwenda kuishi maisha yake kwa uhuru.