Ajifungua watoto pacha akiwa na miaka 73

0
378

Mangayamma Yaramati, Mwanamke mwenye umri wa miaka 73 katika jimbo la Andhra Pradesh nchini India, amejifungua watoto wawili pacha wa kike.

Wauguzi waliomsaidia Mangayamma kujifungua wamesema kuwa, amejifungua kwa njia ya kuanguliwa kwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadaye kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi yaani IVF kwa lugha ya kitaalamu.

Mangayamma amesema kuwa yeye na mumewe ambaye ana umri wa miaka 82, kwa muda mrefu wametamani kupata watoto, lakini hawakuwahi kupata hadi sasa.

Ameongeza kuwa katika muda wote wa ndoa yao, alihisi kutengwa na jamii na wanakijiji wenzake na mara kwa mara amekuwa akitengwa katika mikusanyiko kwa sababu yeye hakuwa mama.