Ajali ya treni yaua 24 DRC

0
434

Watu 24 wengi wao wakiwa watoto wamekufa na wengine Thelathini wamejeruhiwa baada ya treni kuanguka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.


Ajali hiyo imetokea kwenye jimbo la Kasai, ambapo polisi wamesema kuwa baada ya treni hiyo kuanguka mabehewa yake yametumbukia katika mto.


Habari kutoka kwenye jimbo hilo la Kasai zinasema kuwa idadi ya watu waliokufa na majeruhi inaweza kuongezeka, kwa kuwa kazi ya uokoaji inaendelea.
Hiyo ni ajali ya tatu ya treni kutokea katika jimbo hilo ndani ya kipindi cha wiki za hivi karibuni.


Habari zaidi kutoka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zinaeleza kuwa ajali nyingi za treni katika Jamhuri hiyo zimekua zikisababishwa na uchakavu wa treni hizo, ambazo nyingi zilianza kufanya kazi miaka ya 1960 na hazifanyiwi matengenezo ya kutosha.