Agongwa na gari akivusha bata

0
278

Mwanaume mmoja nchini Marekani amefariki dunia baada ya kugongwa na gari, alipokuwa akiwasaidia bata kuvuka barabara.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Rocklin, California ambapo Casey Rivara (41), aliacha gari yake na kwenda kuwasaidia bata hao kuvuka barabara.

Inasemekana Rivara alifanikikiwa kuwavusha bata hao salama kabla ya kugongwa na gari.

Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kufuatia tukio la kugongwa kwa Rivara na uchunguzi bado unaendelea.

Watu mbalimbali wamekuwa wakiweka maua pamoja na picha za bata katika eneo lilipotokea ajali hiyo, ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Rivara kwa wema wake.