Afya ya Malkia Elizabeth II yadhoofika

0
636

Wanafamilia wa karibu wa Malkia Elizabeth II wamekusanyika kwenye Kasri la Balmoral nchini Scotland baada ya afya ya Malkia huyo kudhoofika na kupelekea madaktari wa Malkia kupendekeza apewe usimamizi wa karibu wa matibabu.

“Kufuatia tathimini ya leo asubuhi ya hali ya kiafya ya Malkia, madaktari wamependekeza abaki chini ya uangalizi wa karibu wa usimamizi wa matibabu”, taarifa ya Buckingham Palace imeeleza