Afrika kuzalisha mpunga maradufu

0
220

Japan imeahidi kuzisaidia nchi za Bara la Afrika ili ziweze kuzalisha mpunga maradufu ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza kando ya mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) unaoendelea katika mji wa Yokohama nchini Japan, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Shinzo Abe amesema kuwa Japan ina Teknolojia ya kisasa inayoweza kufanikisha jambo hilo.

Amesema kuwa lengo la Japan ni kuona nchi za Afrika zinazalisha Tani Milioni 50za mpunga katika kipindi cha miaka 11 ijayo.

Kauli ya Waziri Mkuu huyo wa Japan imeungwa mkono na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina ambaye amesema kuwa, hatua hiyo ya Japan ya kuzisaidia nchi za Bara za Afrika kuongeza uzalishaji wa mpunga itasaidia kupunguza njaa katika baadhi ya maeneo ya Bara hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya chakula na lishe ya mwaka 2019, zaidi ya watu Milioni 250 katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika walikabiliwa na njaa katika kipindi cha mwaka 2018.