Idara ya Kilimo, Misitu na Uvuvi nchini Afrika Kusini imethibitisha uwepo wa nzige wa jangwani katika mkoa wa North West, eneo la Karoo pamoja na nchini Namibia.
Katika taarifa yake Idara hiyo imeahidi kupambana na kudhibiti ongezeko la nzige hao kwa kutumia aina Sita za dawa za kuua wadudu ambazo tayari wanazo.
Imekiri kuwepo kwa nzige hao wa jangwani ambao wamekua wakiharibu mazao na kwamba kuwepo kwa nzige hao hakuna uhusiano wowote na wale waliovamia nchi za Kenya, Ethiopia na Sudan.
