Abiy apongezwa na Viongozi mbalimbali

0
1001

Viongozi mbalimbali Duniani wameendelea kutoa pongezi kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, – Abiy Ahmed baada ya kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2019.

Miongoni mwa Viongozi waliotoa pongezi hizo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, Rais Mohamed Farmaajo wa Somalia, Rais Nana Akufo – Addo wa Ghana, Rais George Weah wa Liberia na Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, – Moussa Faki Mahamat.

Abiy mwenye umri wa miaka 43, ametunukiwa tuzo hiyo huko Oslo nchini Norway na kuwa Muafrika wa 12 kutunukiwa tuzo hiyo ya amani ya Nobel.

Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na jitihada zake za kuhamaisha amani na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na kufanikisha kusainiwa kwa makubaliano ya amani mwaka 2018 kati ya Ethiopia na Eritrea baada ya nchi hizo kuwa na mgogoro wa mpaka uliodumu kwa takribani miaka Ishirini.

Abiy alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia mwezi Aprili mwaka 2018, na tangu ashike wadhifa huo amekua akifanya mageuzi mengi nchini humo yenye manufaa kwa Taifa hilo.