Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed hii leo amepokea rasmi tuzo ya Amani ya Nobel mjini Oslo, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuutatua mzozo wa mpaka na nchi jirani ya Eritrea.
Akielezea sababu za kuchaguliwa waziri mkuu huyo, mwenyekiti wa kamati ya Nobel Berit Reiss-Andersen amesema Kamati ya Nobel ya Norway imeamua kumtunuku tuzo ya amani ya Nobel, waziri mkuu Abiy Ahmed Ali kwa juhudi zake za kutafuta amani na ushirikiano wa kimataifa na hasa kuupatia ufumbuzi mzozo huo wa mpakani pamoja na kanda yote ya kaskazini mashariki mwa afrika.
Abiy Ahmed mwenye umri wa miaka 43 ni mshindi wa kumi wa Tuzo ya Amani ya Nobel barani Afrika ambapo
mshindi wa kwanza kutoka afrika alikuwa Albert Luthuli alyepata tuzo hiyo mnamo mwaka 1960 kwa sera yake ya amani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
