Senegal waendelea kupiga kura

0
638

Raia wa Senegal leo wanapiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo.

Rais Macky Sall anayewania muhula wa pili wa uongozi, anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo.

Watu milioni 6.5 wamejiandikisha kupigia kura, na matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa.

Duru ya pili ya uchaguzi huo itafanyika Machi 24 mwaka huu ikiwa hakutakua na mgombea aliyeshinda kwa wingi wa kura.