Whozu alamba dili la mamilioni China

0
1723

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Whozu amesaini mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya TOO MUCH MONEY inayoongozwa na kaka yake Frank pamoja na Fred yenye makao yake Guangzhou, China.

Whozu ambaye kwa sasa anatamba na vibao vyake kama Doko,Roboti, Huendi mbinguni bila kusahau ngoma alioshirikishwa na mwanamitindo Hamisa Mobetto inayoitwa Sensema

Mkataba huo unahusisha Kusimamia kazi za Muziki, vichekesho pamoja na biashara ambazo zitahusisha jina la msanii Whozu ambaye tayari amelipwa USD 30,000 kama malipo ya awali katika mkataba huo.

Akiwa nchini China, Whozu amefanya kazi mbalimbali ikiwemo kurekodi nyimbo na Producers wa China wenye asili ya Nigeria pamoja na kufanya video tatu.