Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kusomewa makosa yanayomkabili ya kusambaza picha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.
Habari zinasema kuwa Wema amefikishwa mahakamani na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).
Hivi karibuni Wema aliwaomba radhi mashabiki wake pamoja na Watanzania wote kufuatia kusambaa kwa picha zake hizo ambazo hazina maadili zilizosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.