Wasanii mbalimbali wa muziki nchini wameendelea kutoa pole kufuatia kifo cha Mwanamuziki wa miondoko ya Hip Hop nchini Golden Mbunda maarufu kama Godzilla aliyefariki dunia ghafla usiku wa Jumatano Februari 13 mwaka huu nyumbani kwao Salasala jijini Dar es salaam.
Kwa sasa mwili wa
Godzilla umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi
ya Lugalo.
Wakati wa uhai wake, Godzilla ametunga na
kuimba nyimbo mbalimbali na atakumbukwa kwa nyimbo zake kama vile Nataka na
Kingzilla.
Godzilla
pia alijizoelea umaarufu na mashabiki wengi kutokana na umahiri wake wa
kuimba mashairi ya papo kwa papo yaani Freestyle.