Wanafunzi Bagamoyo wanufaika na tamasha la Sanaa

0
2002

Baadhi ya Wanafunzi wa shule za msingi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na wale wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa), wamesema kuwa wamenufaika na tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linaloendelea chuoni hapo.

Wakizungumza na TBC Wanafunzi hao wamesema kuwa, wakati tamasha hilo lililoandaliwa na TaSUBa likiendelea, tayari wamejifunza masuala mbalimbali ya sanaa pamoja na yale ya utamaduni.

Tamasha hilo limeingia siku ya Tano hii leo, ambapo Sanaa mbalimbali zimekua zikioneshwa ikiwa ni pamoja na sarakasi, uchoraji, ngoma, maigizo na nyimbo za makabila.

Tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilifunguliwa Oktoba 19 mwaka huu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na linatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 26 mwaka huu.