Wakongwe wa Taarab kuchangia watoto njiti

0
381

Wanamuziki wakongwe katika tasnia ya muziki wa Taarab hapa nchini wanatarajia kufanya tamasha kubwa lililopewa jina la Raha za Pwani 2023, kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto njiti visiwani Zanzibar.

Wasanii hao wakiongozwa na Khadija Kopa, Sabaha Salum Muchacho, Leyla Rashid na Mc Du, watapanda jukwaani Machi 11, 2023 na fedha zitakazopatikana zitanunua vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti huko Zanzibar.

Mwanzilishi wa taasisi ya Doris Mollel inayoshughulika na masuala ya kusaidia watoto njiti, Doris Mollel amesema, wanashirikiana na mwana mitindo wa siku nyingi wa hapa nchini Khadija Mwanamboka katika kuandaa tamasha hilo ili kupata fedha za kusaidia watoto njiti visiwani Zanzibar.