Shishi Food Dar yafungwa

0
293

Msanii na mfanyabiashara Zuena Mohamed maarufu Shilole ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa Shishi Food amesema, mgahawa wa Dar es Salaam umesimamisha shughuli zake za kutoa huduma ya chakula na vinywaji ili kupisha ujenzi wa kituo cha afya ambao tayari umeanza.

Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho umeanza pembeni mwa eneo ulipokuwa mgahawa huo lililopo karibu na viwanja vya Leaders, Kinondoni.

Shishi amewaambia waandishi wa habari
“Ni tamko rasmi kwamba Shishi Food kuanzia leo huduma zitakuwa hamna ili kupisha ujenzi wa kituo cha afya, namshukuru mkuu wa mkoa Amos Makalla, Kaka yangu mkuu wa wilaya Gondwe kwa kunisaidia kufanikisha kupata eneo jingine la biashara, msiache kunisuport eneo lingine tutakaloenda kufanya ujenzi, Mungu anisaidie.” amesema Shilole

Mpaka sasa Shilole amepewa siku tatu kuhamisha na kuondoa kila kitu kwenye eneo hilo.