Gwiji wa tenisi Serena Williams amethibitisha kuwa ana ujauzito wa mtoto wa pili akiwa kwenye onesho la mitindo ya mavazi la MET Gala siku ya Jumatatu.
Bingwa huyo mara 23 wa Grand Slam amewaambia waandishi wa habari katika onesho la mitindo la New York kuwa walikuwa watatu kwenye zulia jekundu alipowasili na mumewe Alexis Ohanian.
Wenzi hao walimkaribisha binti yao wa kwanza, Olympia, mnamo Oktoba 2017.
Williams aliandika katika jarida la Vogue mwaka jana kwamba alitaka kuachana na tenisi na kulenga zaidi kukuza familia yake.