Mwanamuziki maarufu wa nchini Marekani, Robyn Rihanna Fenty maarufu Rihanna na mpenzi wake ambaye ni Rapa A$AP Rocky wanatarajiwa kupata mtoto wao wa pili.
Rihanna anatarajiwa kupata mtoto huyo wa pili ikiwa imepita takribani miezi tisa baada ya kupata mtoto wake wa kwanza ambaye ni wa kiume Mei 13 mwaka 2022.
Akizungumza wakati wa mapumziko kwenye shoo ya Super Bowl hapo jana kwenye uwanja wa State Farm huko Arizona, Rihanna mwenye umri wa miaka 34 aliweka wazi kuwa kuna mgeni maalum ambaye hakutarajiwa.
Katika mahojiano wiki iliyopita, aliulizwa kama kutakuwa na mambo ya kushangaza wakati wa shoo hiyo jana, ambapo Rihanna alijibu “nafikiria kumleta mtu, sina hakika tutaona”.