Rihanna amwagana na Hassan Jameel

0
1065

Mwanamuziki Robyn Fent maarufu kama Rihanna au Badgalriri  ameachana na Bilionea kutoka Saudi Arabia, Hassan Jameel baada ya wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takribani miaka mitatu.

Kwa mujibu wa ripoti za baadhi ya mitandao mikubwa nchini Marekani kama Us Weekly, inaripotiwa kuwa penzi hili la siri limefika mwisho kwa sasa.

Hassan Jameel ni Mfanyabiashara anayetoka kwenye familia tajiri sana duniani, familia yao inathamani ya Paundi Bilioni 1.1 na jarida la Forbes linawataja kuwa familia ya 12 ya Kiarabu tajiri zaidi duniani.

Ukimtoa Hassan alieweza kudumu na Riri miaka mitatu Rihanna aliwahi kuwa na mahusiano na mastaa kama Drake, Chris Brown, Travis Scott na Leonardo Dicaprio.