Msanii wa bongo fleva Tanzania na mmiliki wa lebo ya muziki ya Next Level @rayvanny ametunukiwa tuzo za #DIAFA zilizotolewa kwenye Falme za kiarabu nchini Dubai kama mgeni wa heshima katika hafla ya ugawaji wa tuzo za DIAFA.
Rayvanny anaweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kiume kutoka Afrika Mashariki kutunukiwa tuzo hiyo ya DIAFA ambapo pia alipata shavu la kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo hizo.
Akipokea tuzo hiyo Rayvanny ameipendekeza tuzo hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan akieleza kuwa ni Rais wa kwanza wa Kike katika historia ya taifa la Tanzania.