Q CHIEF ATAMBULISHA NYIMBO ZAKE TATU NDANI YA TBC ONLINE

0
1673

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Aboubakar Katwila Maarufu Q Chief ametambulisha nyimbo zake tatu ndani ya TBC Online huku akiwataka mashabiki wake kumuunga mkono kwa kununua kazi zake.

Q Chief ambaye ameshirikiana na Msanii Mwingine wa Bongo Flaver Harmonize kutoka Kundi la WCB ameachia nyimbo tatu ambazo ni My Boo, Nioneshe na Golo na tayari zinapatikana katika mitandao mbalimbali.

Akiwa katika Studio za TBC, Q Chief ametambulisha Nyimbo hizo kwa mashabiki wake na kuwataka kumuunga mkono kwa kununua kazi zake na kupata ladha ya muziki wake aliomshirikisha nyota wa WCB Harmonize.