Nguli wa Muziki nchini Tanzania, Joseph Haule, maarufu Professor Jay amemshukuru Mungu akisema kwamba sasa yupo imara na anaendelea vizuri sana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemshukuru pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kugharamia matibabu yake ndani na nje ya nchi, pamoja na viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi ambao walifika kwa wingi kumjulia hali.
Aidha, ameushukuru uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vyombo vya habari, Watanzania pamoja na familia yake kwa kusimama nae wakati wote akipatiwa matibabu.
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu mke wangu (@Mke_wa_profjize), kaka zangu, dada zangu Wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mliomipa,” ameandika.
Wasanii na wananchi kwa ujumla waliacha jumbe zao kwenye chapisho hilo wamemshukuru Mungu kuonda nguli huyo akiendelea vizuri, huku wakimtakia siha njema.