Ommy Dimpoz atinga Marekani kushuhudia mechi za NBAAllstar 2020

0
1393

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz kwenye picha ya pamoja na rapper wa Kundi la Migos la nchini Marekani, Quavo Huncho.

Vilevile Ommy amekutana na mrembo Pia Wurtzbach ambaye ni Miss Universe 2015.

Dimpoz amekutana uso kwa uso na watu hao maarufu baada ya kuhudhuria mchezo wa #NBAAllStar 2020 mjini Chicago Marekani.

Dimpoz alisafiri Alhamisi hii kuitikia mualiko huo wa NBA kuiwakilisha Tanzania katika michezo itakayofanyika kuanzia Februari 14 – 16 Mwaka huu mjini humo.