Ni Liverpool vs RB Leipzig, Man City vs Borussia Monchengladbach

0
208

Droo ya 16 bora ya mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya imetangazwa rasmi mara baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi wiki iliyopita.

Chelsea watakutana na Atletico Madrid ambao ni vinara wa ligi ya Uhispania, – Laliga, Liverpool watakutana na RB Leipzig.

Manchester City itasafiri kwenda Ujerumani kumenyana na Wajerumani Borussia Monchengladbach

Vita ambayo inasubiriwa kwa hamu ni vita ya Neymar dhidi ya Lionel Messi ambapo  Barcelona watakipiga na Paris Saint-Germain ambapo mara ya mwisho timu hizo kukutana Barcelona waliwatoa Paris Saint- Germain kwa kipigo cha goli sita kwa moja.

Mechi nyingine ni Real Madrid watakaowakabili Atalanta, Sevilla atakipiga na Borrusia Dortmund na Juventus wakutana na Porto ya nchini Ureno.

Mabigwa watetezi wa mashindano hayo ya Klabu Bingwa Barani Ulaya kwa mwaka 2019/2020 Bayern Munich watachanga karata zao kwa mara nyingine tena  kuelekea kutetea ubingwa wao dhidi ya Lazio ya nchini Italia

Mzunguko wa 16 unatarajiwa kufanyika mwezi Februari na Machi mwaka 2021.