Nandy Festival yaahirishwa

0
2464

Waandaaji wa tamasha la Nandy Festival 2022 wametangaza kuahirisha tamasha hilo kutokana na hali ya kiafya ya mwanamuziki Nandy ambaye ni mwanzilishi wa tamasha hilo.

Taarifa iliyotolewa na waandaji wa Tamasha hilo imeeleza kuwa mwaka huu hakutakuwa tena na tamasha hilo mpaka mwaka 2023.

“Tunasikitika kuahirisha tamasha la Nandy Festival katika mikoa iliyobaki, hii inatokana na hali ya kiafya ya Nandy ambaye ndio mwanzilishi wa tamasha hili” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.