Mwigizaji Lance Reddick afariki dunia

0
435

Lance Reddick, mwigizaji maarufu katika filamu za The Wire na John Wick amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60.

Nyota huyo ambaye pia alikuwa mwanamuziki alifariki kifo cha asili mapema Ijumaa nyumbani kwake jijini Los Angeles nchini Marekani.

Katika siku za karibuni alikuwa katika ziara za kuitambulisha filamu ya nne ya John Wick ambayo inatarajiwa kutoka Machi 24 mwaka huu akiwa mmoja wa waigizaji walioshiriki.

Tamthilia ya The Wire iliyoruka kuanzia mwaka 2002 hadi 2008 ilimtambulisha katika ulimwengu wa filamu, tasnia aliyoitumikia kwa miaka 25.

Reddick ameacha mke mmoja na watoto wawili.