Mwigizaji Jussie Smollett kutoka nchini Marekani amesimama na kupayuka mahakamani kwamba hana hatia baada ya mahakama kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha siku 150 jela.
Mahakama imemtia hatiani mwigizaji huyo aliyeigiza kwenye tamthilia ya Empire kwa makosa ya kudanganya polisi kwamba ni mwathirika wa shambulio la chuki na ubaguzi wa rangi.
Aidha, kifungo hicho kinahusisha miezi 30 ya kuwa chini ya uangalizi pamoja na shilingi milioni 335 ya faini na hasara iliyopatikana.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa, Smollett ambaye ana miaka 39 amesisitiza kwamba hakudanganya katika taarifa aliyoitoa miaka mitatu iliyopita kwamba alishambuliwa na watu wawili.