Mwanamuziki Manu Dibango afariki dunia baada ya kuugua Corona

0
1513

Nyota wa muziki wa Afro Jazz kutoka nchini Cameroon, Manu Dibango amefariki dunia, baada ya kuugua homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Kifo cha Manu Dibango aliyekuwa na umri wa miaka 86 kimetangazwa na familia yake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Dibango amefariki dunia katika hospitali moja iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa alipokuwa akipatiwa matibabu.

Wiki iliyopita alijitangaza kuwa ameambukizwa virusi vya corona.