Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,- Déni Bonet yupo nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja ambapo pamoja na mambo mengine amefundisha kundi la muziki la Stone Town Rockerz.
Nchini Marekani, Déni ameshawahi kufanya kazi na Wasanii kama Cyndi Lauper, R.E.M na Sarah McLachlan na pia ameshawahi kutumbuiza Umoja wa Mataifa na katika Ikulu ya Marekani.
Déni ambaye amekuja Tanzania kwa mwaliko wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini kupitia
Kitengo cha mambo ya utamaduni, amekua akilifundisha kundi hilo la muziki la Stone Town Rockerz uandishi wa muziki na namna ya kutumia vifaa mbalimbali vya muziki.
Kundi hilo linapiga muziki wa taratibu, Jazz ya Kiafrika na kufoka, na pia linatumia lugha za Kiswahili, Kiingereza na zike za Makabila mbalimbali.
Kundi hilo linaundwa na Wanamuziki Salum Matata, Erasto Wambura, Christophe Kagoda, Salum Salem, Alex Migire na Richard Cherehani.