Mwanamitindo Bella Hadid ndiye Mwanamke mzuri zaidi Duniani

0
2092

Utafiti wa Kisayansi kuhusu masuala ya uzuri (Golden Ratio Of Beuty Phi) umetoa orodha ya Wanawake Kumi wazuri Duniani.

Katika orodha hiyo, Mwanamitindo Bella Hadid ametangazwa rasmi kuwa ndiye Mwanamke mzuri zaidi Duniani na kuwapita warembo wengine ambao ni Beyonce Knowles, Amber Heard, Ariana Grande, Tylor Swift, Kate Moss, Scarlett Johansson, Natalie Portman, Katy Perry na Cara Delevingne.

Utafiti huo ambao kwa muda mrefu umekua ukitumiwa na Wanasayansi nchini Ugiriki ili kuwapata Wanawake Wazuri, umekua ukitolewa kwa kuangalia zaidi vigezo vya uzuri wa umbo, midomo, pua, shingo, nyusi, kidevu, taya na umbo la sura.

Bella mwenye umri wa miaka 23, ametangazwa kuwa Mwanamke mzuri zaidi Duniani kufuatia matokeo ya Utafiti huo wa Kisayansi kuhusu masuala ya uzuri kuonyesha kuwa amepata alama nyingi za uzuri katika uso wake, macho, nyusi, pua, midomo, kidevu, taya na umbo la sura.

Ariana
Beyonce

Mwanamuziki Beyonce, yeye ametajwa kuwa Mwanamke wa Pili kwa uzuri Duniani.