Muigizaji Idris Elba apata Corona

0
1562

Muigizaji maarufu wa filamu duniani Idris Elba ambaye pia amewahi kutajwa na jarida la “People Magazine kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani amethibitika kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Kupitia ukurusa wake wa Twitter amechapisha video fupi akiwa na mkewe akizungumza alivyopata maambukizi hayo, na maendeleo ya afua yake.

Elba amesema licha ya kwamba hakuwa na dalili za homa ya mapafu, COVID-19, lakini alipima baada ya kubaini kuwa alikuwa karibu na mtu mwenye maambukizi.

Aidha, ameweka wazi kuwa anaendelea vizuri na kwamba tayari amejitenga ili kuhakikisha hasambazi virusi hivyo kwa watu wengine.