Joseph ‘Jo’ Mersa ambaye ni mjukuu wa mwimbaji nguli wa rege ulimwenguni, Hayati Bob Marley, amefariki dunia.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ambao ni miongoni mwa vyombo vya kwanza kutoa taarifa ya kifo hicho, Joseph, maarufu Jo Mersa, alifariki Jumanne Desemba 27, 2022 kutokana na matatizo yanayohusiana na pumu, ingawa maelezo ya kina kuhusu kifo chake bado hayajawekwa wazi.
Joseph, ambaye ni mtoto Stephen Marley, muda mchache uliopita alijiunga na chuo cha Miami Dade kusoma uhandisi wa sauti (audio engineering).
Mwaka 2014 aliachia EP yake iliyoitwa ‘Comfortable,’ ambayo ilikuwa na nyimbo kama vile ‘Rock and Swing’ na ‘Bogus.’ Pia alitoa wimbo uliovuma sana, ‘Burn It Down,’ mwaka wa 2016 na mwaka jana alifanikiwa kualiachia EP yake ya pili inayoitwa ‘Eternal.’