Miss World kwa mwaka 2018/2019 aitembelea Tanzania

0
1945

Mrembo wa Dunia (Miss World) kwa mwaka 2018/2019 Vanessa Ponce De Leon akiwa katika picha ya pamoja na Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2019/2020 Sylivia Bebwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, – Mrisho Gambo.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha, ambapo akiwa mkoani humo kwa kushirikiana Sylivia, watazindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zitakazojulikana kama Uhuru Pads.


Hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia Taji la urembo la Dunia 2018/2019 kuitembelea Tanzania.


Vanessa anashikilia taji la Urembo la Dunia hadi hapo litakapofanyika shindano lingine la kumpata mrembo wa Dunia, shindano linalotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu nchini Uingereza.