Mamia wajitokeza kwenye mnada wa bidhaa za Chris Brown

0
1743

Mwanamuziki wa miondoko ya R&B anayetikisa dunia kutoka nchini Marekani, – Chris Brown, amefanya mnada wa mauzo ya bidhaa zake ambazo amekwishazitumia ama kuzivaa ikiwa ni pamoja na nguo na viatu.

Mnada huo wa siku Mbili unafanyika katika eneo la nyumba yake mjini Los Angeles, ambapo kabla alituma vipeperushi kwa ajili ya kutangaza kufanyika kwa mnada huo kupitia akaunti zake mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.

Katika vipeperushi hivyo, nyota huyo wa R&B nchini Marekani aliwajulisha watu wanaovutiwa kununua bidhaa zake kufika nyumbani kwake mapema ili waweze pia kuhudumiwa mapema “First Come First Served “, huku vipeperushi vingine vikiandikwa “Yard Sale” ikimaanisha eneo la nyumba yake ambapo mnada unafanyika.

Vipeperushi hivyo vimewawezesha Mamia ya mashabiki wa Chris kujitokeza, wakiwemo wale wanaonunua bidhaa hizo kwa lengo la kwenda kuziuza kwa wengine na wale wanaotaka kuzitumia wenyewe.

Kwa sasa Chris ana albamu yake mpya iitwayo Indigo ambayo inafanya vizuri na kushika hadi namba Moja kwenye chati nyingi za muziki wa Marekani yani Billboard.