Makamu wa Rais wa Marekani atoa orodha ya wasanii wa Tanzania anaowasikiliza

0
768

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ametoa orodha ya nyimbo 25 anazosikiliza wakati akiwa barani Afrika kwenye ziara nchini Ghana, Tanzania na Zambia.

Katika orodha hiyo yenye mahadhi ya nyimbo zenye jumbe mbalimbali Kamala pia amejumuisha wasanii kadhaa kutoka Tanzania.

Miongoni mwao ni Harmonize (Single Again), Jux, Marioo, Papi Cooper & Tony Duardo (Nice Kisee), Zuchu (Utaniua), Alikiba (Mahaba), Jay Melody (Sawa), Mbosso feat. Costa Titch & Alfa Kat (Shetani) na Darassa feat Bein (No Body).

Kiongozi huyo namba mbili wa Marekani anatarajiwa kuwasili nchini Machi 29 hadi Machi 31 mwaka huu.