Maandalizi ya tamasha la Wizkid London yapamba moto

0
2094

Msanii wa Muziki kutoka nchini Nigeria, – Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kwa jina la kisanii Wizkid ama Star Boy, anaendelea kung’ara kwenye chati za Billboard kupitia nyimbo zake mbalimbali.

Kwa sasa Wizkid yuko katika hatua za mwisho za maandalizi ya tamasha lake la Starboy litakalofanyika hivi karibuni jijini London nchini Uingireza kwenye ukumbi wa The O2 ambao una uwezo wa kuingiza watu Elfu Ishirini kwa wakati mmoja.

Tamasha kama hilo pia linatarajiwa kufanyika jijini Paris nchini Ufaransa.

Habari zaidi kutoka jijini London zinaeleza kuwa, hadi kufikia sasa, tiketi zote kwa ajili ya Mashabiki watakaosimama wanaotaka kuingia ndani ya ukumbi huo kwa lengo la kumuangalia Wizkid zimeuzwa na kumalizika.

Tamasha hilo la Starboy litapambwa na Wasanii wengine kama Tiwa Savage, Firebay DML, Afro B, Nafe smallz, DJ Tunez, Juls Baby na Siobhan Bell.

Akiwa katika jiji hilo la London mwaka 2017, Wizkid aliweka historia kwa kuujaza ukumbi mwingine wa Royal Albert.

Kwa sasa Wizkid anatamba na wimbo wake mpya wa Joro ambapo kabla ya wimbo huo, alikua akitamba katika chati za Billboard na wimbo mwingine wa Brown Skin Girl alioshirikishwa na Beyoncé Knowles unaoshika nafasi ya Sita.

Wimbo wake mwingine wa Ghetto Love pia ulitamba kwenye chati hizo mwezi uliopita wa Septemba na kuendelea kumuimarisha zaidi katika muziki.