Kizz Daniel akamatwa na polisi, tamko latolewa

0
2904


Mwanamuziki Kizz Daniel aliyejizolea umaarufu kupitia wimbo wa ‘Buga’ anashikiliwa na polisi Tanzania baada ya kushindwa kutumbuiza katika tamasha la ‘Summer Amplified’ hapo jana Agosti 7 jijini Dar es Salaam.

Inasemekana alishindwa kutumbuiza kwakuwa alikosa nguo baada ya kusahau begi lake la nguo nchini Kenya.

Kampuni ya Str8up, waandaaji wa tamasha la Summer Amplified lililofanyika jana mkoani Dar es Salaam, imesikitishwa na kitendo cha kutotokea kwenye tamasha hilo.

Uongozi wa kampuni hiyo umetoa tamko na kuwaahidi mashabiki ambao tayari walinunua tiketi ili kwenda kumuona mwanamuziki huyo maarufu kuwa, wanalifanyia kazi suala hilo na suluhisho litapatikana.

Katika tamasha hilo ambalo Kizz Daniel alipaswa kutumbuiza, tiketi za kawaida ziliuzwa kwa shilingi elfu 80 na kwa upande wa VIP ziliuzwa kwa shilingi laki moja na nusu.

Hadi tamasha hilo linamalizika, Kizz Daniel alikuwa hajapanda jukwaani, kitendo kilichosababisha vurugu na waandaaji hao kampuni ya Str8up kupokea malalamiko mengi ya kutokuwa na imani nao pamoja na matusi, wengine wakidai warejeshewe pesa zao.

Baadhi ya watu wamesema kuwa si mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kufanya kitendo hicho.