Kayumba: Sikupewa zawadi yote BSS

0
266

Mwanamuziki Kayumba amesema kuwa hakupata stahiki zake zote baada ya kushinda shindano la kusaka vipaji (Bongo Star Search) mwaka 2015.

Akizungumza ndani ya Jaramba Serebuka, Kayumba ameongeza kuwa, changamoto kubwa ndani ya shindano hilo ni kuwa mtu anapewa fedha (zawadi milioni 50) ambayo hajawahi kushika, lakini hasaidiwi namna gani anatakiwa kutumia.

Aidha, amesema katika tamasha hilo kujua kuimba sio kigezo pekee cha ushindi kwani pia inaangaliwa mtu gani akipewa fedha hizo zitaweza kumtoa sehemu moja kwenda nyingine.