Jafo ataka Tamasha la JAMAFEST litumike kuuza Kiswahili

0
2465

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, ametembelea Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea jijini Dar es salaam.

Akiwa katika Tamasha hilo, Waziri Jafo amesisitiza litumike kuuza lugha ya Kiswahili kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mambo mbalimbali yanafanyika wakati wa Tamasha hilo ikiwa ni pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa Wasanii mbalimbali, Nyama Choma, pamoja na maonesho ya bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali.

Tamasha hilo linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, lilizinduliwa rasmi Septemba 22 mwaka huu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.