Hatimaye mashabiki wa Mwanamuziki Ja Rule kutoka Marekani, watapata nafasi ya kuona video za nyimbo za Mwanamuziki huyo kama Free, Where I’m from, Passion na Better days.
Hii ni baada ya Ja kutangaza kuwa ataachia video za nyimbo zote alizowahi kuziimba.
“Nitaachia tena album zangu zote kama video, nitatengeneza video ya kila ngoma niliyowahi kurekodi, Ngoma gani unatamani kuona nikiachia video yake kwanza?, ” ni maneno ya Ja Rule aliyoyaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Ja Rule pia amepanga kuachia album yake mpya aliyoipa jina la Twelve ikiwa ni album yake ya kwanza tangu ile ya mwaka 2012 Pain is Love 2.